Unaweza ukauambia moyo wako "Kama nikivaa majukumu ya mwenzangu na kuwajibika vilivyo, kumchukulia kutokana na yeye alivyo na yeye pia akafanya hivyo hakika tutadumu"
Kuvaa majukumu ya mwenzako Ni moja ya dawa ya kutatua/ kudumisha mahusiano.Jukumu la kumpenda, jukumu la kumpa furaha, jukumu la kumshauri,kumvusha katika shida na dhiki mbalimbali, jukumu la kumvumilia, n.k. Maana nyingne ya mahusiano Ni ushirikiano hivyo kupitia hili mnaweza kuwa watu wa tofauti na mnaweza mkafanya Mambo makubwa kuliko kawaida na mkafurahiana.
Vaa jukumu la kumvumilia mwenzako.Wengi hushindwa kuendelea na wapenzi wao kwa kushindwa kuvumilia tabia zao/vile walivyo.Kazi ya uvumilivu sio sawa na upendo,upendo kazi yake ni kuimarisha mahusiano lakini uvumilivu kazi yake kudumisha mahusiano na huwezi kuimarisha kisichodumishwa! Tutakuja kuona hapo baadae faida za uvumilivu katika mahusiano.Kuwa tayari kuvumilia kwa Mambo mbalimbali yanayotokea katika mahusiano yako.
Vaa jukumu la kubadilika pale unapoambiwa kosa lako na mwenzi wako,ukifanya hivi unaonyesha kupenda,kujali na kujali afya ya mwenza wako, atakupurahia na mtafurahiana.
Kama una shamba zuri Lina udongo mzuri na wenye rutuba huwezi tazama,kufikiria,kutamani shamba usilojua uimara wake.
#Imarisha mahusiano#

1 Comments
Thanks bby umenisaidia alot
ReplyDelete