Tafiti zinaonyesha asilimia kubwa ya watu ambao wapo kwenye mahusiano ya muda mrefu( wamedumu kwa muda mrefu), Kuna wakati ukifika huwa wanachokana. Na hii huletwa na kuzoeana, yaani unaishi naye kwa mazoea, na huu ni wakati ambao mtu hupoteza msisimko katika mahusiano.

Dalili za kupoteza msisimko katika mahusiano ni Kama vile; Kutokua na hisia naye hata akikushika mahali popote, akipiga simu/akikutumia meseji unaona lakini hupokei Wala hujibu meseji, haumkumbuki hata akiwa mbali kwa muda fulani, ukimuona haumfurahii, hata akitumia lugha ya upole unahisi kama anaongea vitu usivyovielewa, kuwa na muitikio hasi akifanya vitu ulivyokuwa ukifurahia zamani( In hot love stage).

Yapo mambo mengi sana yanayo onyesha kupotea kwa msisimko katika mahusiano. Leo utaweza kufahamu namna ya kumfurahia mwenzi wako na kuyafanya mahusiano yawe mapya kila asubuhi. 


1. Muone mpenzi wako ni rafiki yako kipenzi(best friend) kuliko mtu yoyote.
      Kuna watu wanaweza kuwa kwenye mahusiano lakini wanaogopana kiasi kwamba hata kuna baadhi ya mambo huwezi kumwambia mpenzi wako,eti unamuogopa, hii ni mbaya Sana.
Mtanie, mueleze jinsi unavyojisikia, nini unataka, kuwa kama mtoto kwake haijalishi una/ ana umri gani,mkiishi kama hivi hamtakuja kuchokana na kila wakati mtakumbukana, hata akiwa mbali atakupigia simu atakwambia "darling nimemiss vituko vyako",deka, jisikie huru,usimuogope, chezeni hata michezo ya kitoto. Ni moja ya msingi mkubwa Sana katika mahusiano.

2. Msome na umuelewe, nini anapenda,nini hapendi.
      Ukimuelewa kwamba mpenzi wangu huwa hapendelei vitu hivi basi hautavifanya na vile anavyovipenda utavifanya zaidi. Hii inakupa uwanja mpana zaidi kwani inakupunguzia migogoro isiyo ya lazima, wasiwasi ndani yako, hukuongezea amani kwasababu unakuwa umemfurahisha mpenzi wako hata yeye pia anakuwa anakufurahia. Usipende kurudia rudia makosa, mara ya kwanza akikwambia hajapenda ulivyofanya basi muelewe na usirudie mara nyingine tena.

3. Pendelea kutumia lugha anayoipenda zaidi.
     Haimanishi lugha za kawaida, bali ni lugha za mapenzi mfano; kumpa zawadi, kutoa muda wako kwajili yake, kumsaidia kazi, kumsaidia n.k. Hii inakusaidia kujenga tabasamu kwa mwenza wako kila wakati hata wewe pia unakuwa na amani ndani yako juu ya hilo.

4. Muamini
      Kuna mtu anaweza akawa na mpenzi lakini hamuamini. Hii Haina haja ya kuendelea naye kama humwamini, kwasababu kwa kila atachofanya utaona kama si cha kweli, hautamfurahia, hautadumu naye. Mwamini mpenzi wako, amini kwamba anakupenda, amini vitu vingi anavyovifanya kwajili yako, mpe muda wa kuzungumza, ajieleze anavyojisikia, msikilize na onyesha kumuelewa kwa vile vitu alivyozungumza.

5. Kama akiwa amechukia(Mpo kwenye mgogoro) tumia lugha/ fanya vile vitu ambavyo kwa mara ya kwanza kabisa alikua akifurahia Sana.
      Mfano; Kuna wakati mlikua mkikaa wawili kuna nyimbo anakuimbia/unamuimbia na hufurahia Sana, michezo fulani fulani mlikuwa mkicheza mnafurahiana, hadithi n.k yapo Mambo mengi ambayo hata wewe unayakumbuka basi pendelea kuyafanya hayo akiwa amechukia.

6. Furahia anachokifanya, msapoti
         Kuna mtu anaweza kuwa na mpenzi wake lakini hajui anajishughulisha na nini au hata Kama anajua basi hauonyeshi mwitikio wowote juu yake. Basi fanya hivi; kwa lolote analofanya mwenzi wako jifunze kumuunga mkono, hata kwa ushauri,kumtia moyo,kama kuna chochote cha kumpa basi mpe ili aone mchango wako katika maendeleo yake, na siku akisimama mbele wa watu/ akishinda atasema " Nampenda Sana mpenzi wangu........(jina) kwasababu ushindi wangu chanzo ni yeye, namshukuru sana''. Atakutaja na utasikika naa kila watakapo muona yeye watakuona wewe.

        Inaendelea.......
            
                 #Imarisha mahusiano#