Moja ya vitu vinavunja ndoa,uchumba au mahusiano kiujumla Ni migogoro. Katika mahusiano migogoro inatokea Sana na ndomana hata wanasema vikombe kabatini navyo hugongana, lakini wengi wamelichukulia hili Kama nafasi ya kuvunja mahusiano yao.

Ni kitu ambacho hakileti maana Sana kumwacha mtu unayempenda/sahihi kwa sababu ya Mambo madogo Sana yanayoweza rekebishwa.

Na ukiona watu ambao wapo kwenye mahusiano na wanaachana sio kwamba walikuwa hawapendani Bali Ni kwamba wamekosa maarifa ya kuishi pamoja.

MAARIFA YA KUISHI PAMOJA
Hii Ni ufahamu,hekima,busara,upendo,uvumilivu, n.k vinavyounganisha na kudumisha wapendanao. Vitu hivi husaidia kutatua migogoro mbalimbali katika mahusiano.

Tafiti zinaonyesha ndoa za watu wengi zinavunjika kwa kusikiliza watu wa nje wanasemaje juu ya mwenza wake au ndoa yake pia kuingizia matatizo binafsi kwa mwenza wake au ndoa yake, na hili Ni tatizo kubwa.

Mwanaume/mwanamke anaweza akatoka kazini, siku hiyo amekasirishwa na wafanyakazi wenzake,amepata hasara katika biashara zake,amejibiwa vibaya na watu Basi anazichukua zile hasira na kuzihamishia kwa mwenza wake, na kufanya mgogoro kuwa mkubwa kiasi kwamba kushindwa kuelewana.

Thaman ya mwenza wako ibaki pale pale, usimlinganishe na watu wengine na hata kuwa na hasira naye katika Mambo yako binafsi.

Mwenza wako ndiye mtu wako wa karibu Sana wa kukupa faraja na amani haijarishi katika nyakati gani. Akirud/Ukirudi toka kazini tengeneza tabasamu ili kuweka mazingira mazuri ya kumweleza namna ulivyopatwa na matatizo naye atajua namna gani ya kukusaidia, lakini ukisema umchukie na mwenza wako Basi unakuwa umeongeza tatizo juu ya tatizo, Basi unakuwa umepoteza kila kitu.

Mthamini mwenza wako katika Hali zote na mwamini kwamba anaweza kukusaidia kukupa faraja katika Hali zote.

               #Imarisha mahusiano#