Utajuaje  kwamba mwanaume anakupenda kwa dhati?
Wasichana wengi huwa wanakuwa na mgogoro wa nafsi pale ambapo, kijana wa kiume amemfata na kumwambia anampenda na ana malengo naye lakini anakuwa haamini kama kweli anampenda na wakati huo anahitaji kumkubali.

Kwa wanaume pia, anaweza kuambiwa na mdada ''nitaaminije kama kweli unanipenda?''. Ni jambo jepesi sana, lisikuumize moyo,akili wala kichwa.

Kama ni msichana ukiona mwanaume anakufanyia hivi basi amini kwamba anakupenda, na kama ni mwanaume ukiona msichana anakuambia haamini kama unampenda basi fanya hivi vifuatavyo;

1. Atakukubali na kukupenda vile ulivyo.
    Haijalishi una mapungufu gani, watu wanazungumzaje kuhusu wewe, lakini yeye moyo wake, umeridhika na una shauku Sana ya kuwa na wewe. Na ndio maana unaweza kuona mdada yupo kwenye mahusiano na mkaka ambaye watu wengi hawampendi/ wanaona kama haeleweki basi wanakuuliza '' huyo mwanaume ulimpendea nini, mbona kama havutii!".Fahamu kwamba utamu wa pipi Ni mate yako na thamani ya mtu uliyempenda unaijua wewe na sio mtu mwingine yoyote. Hivyo ukiona mambo kama haya, ujue huyo mtu anakupenda kwa dhati, pia atakulinda Kuna msemo unasema " Kama kweli unampenda utamlinda''

2. Atakuweka/ atakupa nafasi ya kwanza/juu mara nyingi. 
        Wengine huwa wanaita "my number one" kwasababu katika mambo mengi amemuweka mstari wa mbele, kumshirikisha mambo yake,mikakati, changamoto, biashara zake, mambo ya familia na hata akiwa sehemu yoyote haijalishi mpenzi wake yupo au hayupo basi atakuwa akimsifia kwa moyo wa upendo kabisa. 
Hadi kufanya hivi anakuwa anakuamini, anakuthamini, anaelewa umuhimu wako.

3. Anakusaidia siku zote( Supportive Man)
           Katika shida, changamoto na mambo mengine mengi atakuwa hapo kukusaidia kwasababu siku zote yeye ni furaha yake kukuona upo kwenye hali ya furaha, hawezi kukuacha katika hali ya machozi, na hapa huwa tunasema "Katika nyakati nzuri wapenzi wako watakujua wewe lakini katika nyakati mbaya utamjua mpenzi wako''. Yaani anayafanya mambo yako kama yake, shida zako kama zake, anauvaa uhusika wako wakati wowote, na yuko tayari kwa lolote ili kukusaidia.

Katika mambo anayotoa msaada kwako kama vile kukuombea, kukushauri, kutumia muda na wewe ili kukuondolea upweke, msaada wa kifedha n.k


4. Huelezea hisia zake kwako mara nyingi.
           Ni mtu ambaye mara nyingi akikuona, akiwa mbali anafikiria kuhusu wewe, na anakwambia namna anavyojisikia  juu yako, na anakuwa amekuamini hata kukuelezea hisia zake kwako. Na hujusikia furaha anapokuwa na wewe siku zote, hata akiwa na wewe siku nzima hachoki na anafurahia matukio kama hayo.

5. Siku zote atakuwepo kukupa furaha na sio kukupa huzuni.
     Kama akikukosea atakuwa wa Kwanza kukuomba msamaha, hatasubiri hadi uonyeshe vile namna umekasirishwa na alichokifanya. Hataruhusu huzuni iwe kwako kirahisi, atakulinda katika kila namna. 


Ukiona mwanaume anayafanya yote haya usipoteze nafasi amini kwamba anakupenda Sana!


Email:dveronika546@gmail.com
WhatsApp: 0765902911
                
                #IMARISHA MAHUSIANO